Skip to main content

CHANGIA

'Wahubirini mataifa habari zake, Na watu wote habari za maajabu yake' (Zaburi 96:3). Tunaamrishwa na Biblia kuhubiri habari za Mungu aliye mbinguni. Blogu hii imelenga kufata maandiko haya. Msomaji unayependwa na Baba shiriki nasi katika kueneza habari za Mungu kwa namna hizi tatu;

1)     Wasambazie watu wengine hasa watu wako wa karibu kuhusu maneno ya Mungu unayoyasoma hapa na kwingineko. Tumia mitandao ya kijamii kutekeleza agizo la Baba aliyekuumba na utabarikiwa duniani na mbinguni. Sema Amen.
  
2)     Jiunge na watumishi wa Mungu wanaoandika habari za Mungu kwenye blogu hii. Ungana na mtumishi Frank Msuya, Steven (Kassim) Zuberi na mtumishi Clara Mwaipopo. Kama una uwezo mzuri wa kuandika makala kuhusu mafundisho ya Biblia basi andika na utume kwenye bibliayetu@gmail.com. Mhariri wetu ataizama na kuichapisha hapa. Hakika utainuliwa. Sema Amen.
  
3)   Changia Tshs 400 (mia nne) tu au zaidi ulivyobarikiwa kwa ajili ya kuihudumia na kuitangaza blogu hii na hakika Mungu atatimiza haja ya moyo wako kwa chochote unachokiomba. Sema Amen. Baadhi ya matumizi ya pesa yako mtumishi wa Mungu ni haya yafuatayo;

Ø  Kwa sasa tunatumia huduma ya bure ya blogu (blogspot) na hivyo haina ufanisi wa kutosha na usalama ni mdogo, kati ya matatizo mengine mengi. Changa ili tuweze kuifanya ijitegemee kwa kuilipia na neno lifike mbali zaidi kote Afrika Mashariki. 
Ø  Fedha zinahitajika kwenye kununua vifurushi vya internet kwa ajili ya kuihudumia blogu na ukurasa wake wa facebook.
Ø  Kulipia matangazo yetu kwenye blogu nyingine, kwenye facebook na magazetini ili watu wayaone na kuja kusoma neno la Mungu.

Tunashukuru waliochanga mbaka sasa na hasa watumishi hawa watatu; Abdon Mushi (Tshs 50,000), Nasra Stephen (Tshs 37,000) na Michael Zebadia (Tshs 25,000). Kwa pesa hizo tumeweza kulipa deni la mtaalamu aliyetengeneza blogu na kuwa na kiasi cha akiba kwenye hazina yetu. Mungu awape zaidi. Amen.

Muwe wepesi kutoa nanyi mtapokea (Luka 6:38). Kama umeguswa toa kwa ajili ya Mungu. Tutumie email kupitia bibliayetu@gmail.com. 

Ni bora kutoa pesa na kuubadilisha ulimwengu kuliko kuilimbikiza ama kuitumia kwenye mambo yamchukizayo Muumba wako. Omba hitaji lolote la moyo wako na Mungu atakutimizia haraka mno kwa sadaka hii. Amen.