Kwanini
unasumbukia maisha ya dunia mbaka unamsahau Mungu aliye mbinguni na neno lake?
Umesahau andiko la Biblia linalokuonya usije kusahau agano la Yehova Mungu wako
ambalo alifanya pamoja nawe? (Kumbukumbu la Torati 4:23). Mungu anasema wala
msisahau agano nililofanya nanyi; msiabudu miungu wengine (2 Wafalme 17:38).
Unaifahamu
miungu mingine unayoiabudu? Pesa, mali, starehe na vingine unavyovitumikia ama
kuvihangaikia ndio miungu mingine. Pengine Biblia iko karibu nawe hapo ulipo.
Fungua Mathayo 6:24. Inasema Biblia kuwa hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana
wawili kwa maana atamdharau mmoja na kumtukuza mwingine. Huwezi kutumikia Mungu
na mali.
Neno
linaendelea kusema kuwa usiwe na wasiwasi kuhusu maisha yako: utakula nini ama
utavaa nini (Mathayo 6:25). Hapa Mungu ana maana ya kwamba yote hayo yapo kwenye
mamlaka yake na huamua yeye ampe nani. Hii haina maana, hata hivyo, kuwa
usifanye kazi kwa maana Biblia bado inasisitiza kazi. Alimaye shamba lake
atakuwa na chakula tele; bali atafutaye mambo ya upuuzi hana ufahamu (Mithali
12:11). Funzo la maana hapa ni kuwa uhangaikie dunia lakini usimsahau baba yako
aliyekuumba.
Fanya
kazi kwa ajili ya maisha ya dunia ewe ndugu lakini muweke zaidi Mungu mbele kwa
maana ndiye anayekupa uwezo wa kufanya kazi. Unaposoma andiko hili kumbuka kuna
mwenzako yupo ndani ya wodi ya hospitali akiwa hana matumaini ya kupona ugonjwa
unaomsumbua. Ana kansa ya damu, kansa ya mapafu ama maradhi mengine makubwa.
Huruma ya Mungu inakufanya wewe kuwa na afya njema na unasoma andiko hili.
Mtukuze baba aliye mbinguni.
Kuwa
karibu na Mungu kutakupa neema zaidi. Lishike neno lake na usilisahau. Usisahau
kusali mara zote uwapo kwenye matatizo na usisahau kumtukuza Mungu na kumsifu
unapojihisi furaha na amani ya moyo wako. Yesu anasema kuwa mnaposali na kuomba
kitu, aminini kwamba mmekipokea nanyi mtapewa (Marko 11:24). Omba kwa maneno
mafupi haya chini kwa imani kwamba Mungu anakwenda kutatua haja yoyote ya moyo
wako hivi karibuni;
‘Mungu
baba najileta kwako nikiwa dhaifu na mnyenyekevu. Hakuna aliye juu yako kwa
maana unautawala ulimwengu. Umenielekeza nikuombe niwapo na shida nami
nimekuja kukuomba bwana Mungu wangu. Niondolee maradhi, umasikini na shida zote
za ulimwengu. Kidhi haja ya moyo wangu, unipe furaha na uniongezee kipato.
Nishindie vita dhidi ya maadui zangu. Amen’
Kwa
sala hiyo Mungu anakwenda kukuondoa kwenye janga lolote ulilo nalo. Mungu
anakwenda kukupandisha daraja zaidi ya wale unaotamani kuwa kama wao. Mungu
anakwenda kukupa afya njema siku zote za maisha yako na kukupa maisha marefu
mithili ya baba yetu Adam. Amen. Ukumbuke kuwa unapompuuza Mungu na neno lake
kwa kuacha kufanya maombi unakuwa umejipuuza mwenyewe.
Usisahau
kushare na wengine waje wasome neno la Mungu kwenye blogu hii inayoendeshwa kwa
ajili ya Mungu. Kwa ajili ya kukumbusha uwepo wa Mungu na kumuabudu. Mungu anakulekeza kwenye Marko 16:15 ulieneze neno lake. Hakika atakutimizia haja kuu ya moyo wako. Amen. Kama umeguswa bofya >>>HAPA<<< kuchangia juhudi zako katika kueneza neno lake, nae Mungu atakuinua. Amen.