“Mtakapoona mambo hayo yanatendeka, mtatambua
kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia” (Luka 21:31). Unayajua mambo hayo
yanayosemwa kwenye mstari huu wa Biblia takatifu. Chapisho hili linakuonesha
mambo hayo ambayo yameshatokea na yanaendelea kutokea na ni dalili za wazi kuwa Yesu
Kristo atarejea hivi karibuni.
Zipo dalili nyingi mno zinazoashiria kuwa punde tu Kristo atashuka tena duniani. Hata hivyo chapisho hili linazungumzia dalili nne kuu ambazo si za kupuuza. Yatupasa tujiandae na ujio wa Masihi kwa kufanya ibada, kutoa sadaka na mengine yampendezayo Bwana. Dalili nne kuwa Yesu anakaribia kurejea ni hizi zifuatazo;
1) VITA
NA TETESI ZA VITA: “Mtasikia habari za
vita na tetesi za vita, msitishike; kwa maana haya hayana budi kutokea; lakini
mwisho utakuwa bado. Taifa kwa taifa na nchi kwa nchi zitapigana…” (Mathayo
24:6, 7a).
Utakubaliana
na mimi kuwa zipo tetesi za kutisha za vita kwa sasa ndani ya dunia hii tangu kuisha kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Namna mataifa makubwa kama Marekani , Korea
Kaskazini na wengine yanavyovutana na kutishiana ubabe wa kijeshi ni tetesi kubwa
mno za vita. Usitishike mtumishi wa Mungu kwa maana haya hayana budi kutokea.
2) NJAA
NA MATETEMEKO YA ARDHI: “Hapa na pale
kutakuwa na upungufu wa chakula na tetemeko la ardhi. Mambo hayo yote ni mwanzo
wa maumivu ya taabu. (Mathayo 24: 7b, 8)
Kwenye
miongo ya karibuni dunia imeshuhudia matetemeko makubwa mno ya ardhi. Tetemeko
la Valdivia (Chile, 1960), Sumatra (Indonesia, 2004) na lile la Port-au-Prince
(Haiti, 2010) ni mifano michache ya matetemeko ya balaa. Pia kwa mujibu wa ripoti
ya Shirika la Chakula Duniani (FAO) ya mwaka 2014 zaidi ya watu miloni 800
duniani hawana chakula cha kutosha.
3) MANABII
WA UONGO: “Na manabii wengi wa uongo
watatokea na kuwapotosha wengi” (Mathayo 24:11)
Duniani
kote miaka hii wanatokea wengi wanaojipa sifa za Masihi kwa namna isiyompendeza
Bwana wakiwa na lengo la kujaza makanisa na kujinufaisha wenyewe. Hawa ndio
manabii wa uongo waliotabiriwa na maandiko ya Biblia. Wapo wengi pia waliodai wazi kuwa wao ni Yesu Kristo. Mmarekani
Maurice Clemmons alijinadi hivyo mwaka 2009 na Muingereza David Shayler
alifanya hivyo mwaka 2007.
4) WANA
WA ISRAEL KUREJEA KWENYE ARDHI YAO: “…Yehova
amesema hivi, “Tazama, nitawachukua wana wa Israeli kutoka katikati ya mataifa
ambako wameenda, nami nitawakusanya kutoka pande zote na kuwaleta katika nchi
yao” (Ezekieli 37:21)
Kabla
ya mwaka 1948 wana wa Israel walikuwa wametawanyika sehemu mbali mbali za dunia
wasiwe na ardhi waliyoiita nchi yao. Kipindi cha Vita Kuu ya Pili ya Dunia
utawala wa Nazi kule Ujerumani uliua takribani wana wa Israel milioni sita.
Hivyo ikaonekana haja ya wao kuwa na ardhi yao. Kwa msaada wa Mungu kupitia kwa
mataifa makubwa wana wa Israel wakapata nchi yao huru mwaka 1948.
Msomaji
unayependwa na Bwana hizi ni dalili za wazi kuwa Masihi yu karibu kurudi. Yesu
alisema kuwa amekwenda kututayarishia wewe na mimi mahali kwenye nyumba ya Baba
ambapo tutakaa na yeye (Yohana 14:1-4). Tunahitaji kufanya ibada, kutoa sadaka
na kutangaza neno lake Bwana ili tupate nafasi ya kwenda kwenye nyumba yake.
Fanyia
kazi neno hili la Mungu naye atakuinua duniani na mbinguni, Amen. Kwa kuwa
Mungu amekupa afya njema na amani mahali ulipo sasa unatakiwa kutumia nafasi
hiyo kujiunga nasi katika kueneza neno lake. Tumia dakika mbili tu kuunga mkono
juhudi hizi kwa kubofya >>>HAPA<<<.