Skip to main content

Posts

Yesu yu karibu mno kurudi: Dalili hizi si za kupuuza

“ Mtakapoona mambo hayo yanatendeka, mtatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia ” (Luka 21:31). Unayajua mambo hayo yanayosemwa kwenye mstari huu wa Biblia takatifu. Chapisho hili linakuonesha mambo hayo ambayo yameshatokea na yanaendelea kutokea na ni dalili za wazi kuwa Yesu Kristo atarejea hivi karibuni. Zipo dalili nyingi mno zinazoashiria kuwa  punde tu Kristo atashuka tena duniani. Hata hivyo chapisho hili linazungumzia dalili nne kuu ambazo si za kupuuza. Yatupasa tujiandae na ujio wa Masihi kwa kufanya ibada, kutoa sadaka na mengine yampendezayo Bwana. Dalili nne kuwa Yesu anakaribia kurejea ni hizi zifuatazo; 1)      VITA NA TETESI ZA VITA: “ Mtasikia habari za vita na tetesi za vita, msitishike; kwa maana haya hayana budi kutokea; lakini mwisho utakuwa bado. Taifa kwa taifa na nchi kwa nchi zitapigana …” (Mathayo 24:6, 7a). Utakubaliana na mimi kuwa zipo tetesi za kutisha za vita kwa sasa ndani ya dunia hii tangu kuisha kwa Vita Ku...
Recent posts

Epuka chuki hata dhidi ya maadui kwa maana chuki humchukiza Mungu

Kila kiumbe aliye duniani  au  hata mbinguni anao  au   amewahi  kuwa na maadui kwenye maisha yake. Ndugu yangu msomaji pengine wapo watu ambao unaamini ni maadui zako. Unajua wazi kuwa hawapendi ufanikiwe. Hujaribu kutafuta namna ya kuhakikisha hufikii malengo yako kwenye maisha ama kile alichokupatia Mungu kinapotea. Kama unao watu hawa hakika ni maadui zako. Unajua la kufanya ndugu  msomaji unayependwa na Mungu? Pambana nao maadui zako lakini kwa njia alizoelekeza Mungu wa mbinguni. Pambana nao kwa upendo kwa maana chuki humchukiza Bwana. Kama adui yako ana njaa mpe chakula; kama ana kiu; mpe kitu anywe maana ukifanya hivyo utampalia mkaa wa moto kichwani pake (Warumi 12:20). Kupalia mkaa wa moto kichwani kwa adui ina maana ya kutoa ‘adhabu ya kiungu’. Hii ni kwa mujibu wa wanathiolojia wakubwa wa kikristo kama Charles Ellicott, Matthew Henry na Albert Barnes. Mpe adhabu ya kiungu adui yako. Adhabu ya kiungu ni ile itakayomfanya ajutie ama...

Usimpuuze Mungu na neno lake: Ukifanya hivyo unajipuuza mwenyewe

Kwanini unasumbukia maisha ya dunia mbaka unamsahau Mungu aliye mbinguni na neno lake? Umesahau andiko la Biblia linalokuonya usije kusahau agano la Yehova Mungu wako ambalo alifanya pamoja nawe? (Kumbukumbu la Torati 4:23). Mungu anasema wala msisahau agano nililofanya nanyi; msiabudu miungu wengine (2 Wafalme 17:38). Unaifahamu miungu mingine unayoiabudu? Pesa, mali, starehe na vingine unavyovitumikia ama kuvihangaikia ndio miungu mingine. Pengine Biblia iko karibu nawe hapo ulipo. Fungua Mathayo 6:24. Inasema Biblia kuwa hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili kwa maana atamdharau mmoja na kumtukuza mwingine. Huwezi kutumikia Mungu na mali. Neno linaendelea kusema kuwa usiwe na wasiwasi kuhusu maisha yako: utakula nini ama utavaa nini (Mathayo 6:25). Hapa Mungu ana maana ya kwamba yote hayo yapo kwenye mamlaka yake na huamua yeye ampe nani. Hii haina maana, hata hivyo, kuwa usifanye kazi kwa maana Biblia bado inasisitiza kazi. Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele...